Monday, June 11, 2007

wanasiasa kandambili

SEHEMU YA I
Ali Mwinyi Msuko


DEMOKRASIA inamaana pana sana katika uwanja wa siasa. Asili ya neno Demokrasia linatokana na lugha ya Kiyunani (Kigiriki) ambalo msingi wake ni maneno mawili DEMO ambalo maana maana yake watu na KRATOS likiwa na maana ya ututawala. Kwa kifupi maana ya neno ni Utawala wa Watu, kwa kumaanisha matakwa ya watu wengi. Na kinyume chake ni “Autocracy” yaani Udikteta. Kwa ufupi Demokrasia maana yake ni wengi wape au kukubali na kuheshimu maamuzi ya wengi. Kwa maana hiyo mtu hawezi kuwa mwanasiasa, bila kuwa mwanademokrasia, lakini inawezekana kuwa mwanademokrasia pasi na kuwa mwanasiasa. Kwa kuwa demokrasia ndio msingi mkubwa wa siasa, hivyo mwanademokrasia anaweza kuwa mwanasiasa mzuri kwa sababu ana msingi madhubuti wa kuelekea kuwa mwanasiasa.

Hata hivyo, mtu anaweza akawa na sifa zote hizo mbili na pia inawezekana akawa hana sifa hata moja katika hizo, lakini akajipa sifa hizo kwa nguvu. Kwa hakika, mwanasiasa mzuri lazima awe pia mwanademokrasia. Mwanasiasa mzuri lazima awe mtu mtaratibu, mpole, mstaarabu na mwenye kushauriana na wenziwe na awe anakubali kukosolewa na kujikosoa. Kubwa zaidi awe mwenye subira na mstahamilivu, kupungukiwa na sifa hizo, ni kukosa muhimili mkuu wa kuwa mwanasiasa.

Mwanasiasa siku zote huwa mkweli na muaminifu anayoyasema hayatofautiani na anayoyatenda Kwa kuwa hao waliojipachika uwanasiasa maneno yao tafauti kabisa na vitendo vyao, basi hatuwezi kuwaita wanasiasa bali ni wababaishaji tu wa siasa.

Nchini Tanzania tangu uanze mfumo wa siasa wa vyama vingi mwaka 1992, karibu watu wengi wamejifanya kuwa wanasiasa na wengine kudiriki hata kuunda vyama vya siasa. Lakini tukiangalia nyendo na vitendo vya watu hao inaonekana wanapenda tu kuwa wanasiasa bila ya kuwa na misingi madhubuti ya uwanasiasa, hivyo wanashindwa hata kukaribia kufikia hadhi hiyo.

Katika kufuatilia kwa karibu nyenendo za baadhi ya wanasiasa wa hapa nchini, imebainika baadhi yao huwa wanatafuta kura za wananchi ili ziwawezeshe kutimiza matakwa yao ya kajipatia umaarufu, maslahi binafsi na katambulika ili waweze kupata madaraka.

Kigezo nakipimo kikubwa cha kumfahamu mwanasiasa, kiko katika kuangalia nyendo zake na kuzilinganisha na misingi ya demokrasia. Misingi hiyo inazingatia Uhuru na Haki, kupinga aina zote za ubaguzi, ama wa rangi, kabila, dini, jinsia au umajimbo na kutoa haki ya kila mtu kushiriki katika mambo ya utawala wa nchi. Jambo la muhimu katika misingi hiyo ni nidhamu, inayolazimisha wacheche wakubaliane na matakwa ya wengi na wengi nao waheshimu maamuzi ya wachache, kila mtu awe na haki kuchagua kiongozi anaemtaka au kuchaguliwa kuwa kiongozi.

Kwa mtazamo huo demokrasia inaweza kuwapo mahali popote, iwe ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa au katika mfumo wa chama kimoja mradi tu, misingi hiyo mikubwa iwe inafuatwa. Hivyo demokrasia nchini Tanzania ilianza tangu enzi ya mfumo wa chama kimoja.

Zanzibar imeshuhudia awamu tofauti za uongozi. Pamoja na yote hayo kumekuwa na baadhi ya watu wanadai ukombozi wa nchi. Swali liliopo ni nani anayetawala Zanzibar hivi sasa? Na ameingia katika utawala kwa njia gani? Jibu lake linaweza kuwa na utata, kwani litahusishwa moja kwa moja na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Na utaambiwa kuwa ulipoanzishwa muungano wananchi hawakushauriwa. Zanzibar imemezwa na Tanzania Bara. Mapinduzi ya Januari 12. 1964 yameiondoa serikali halali ya Sultani. Na mengi mengine.

Kutakana na majibu ya aina hiyo ndipo hoja ya kusema kwamba kuna watu wanapeda kujiita wanasiasa na wakati wakiwa hawana sifa hiyo, inapopata nguvu. Kwani mwelekeo wa watu hao sio kujenga Taifa lenye nguvu, bali ni kudhofisha na kuleta mgawanyiko miongoni mwa jamii ya wazanzibar na watanzania katika kipindi hiki, kwani wanaposema wanataka kuikomboa Zanzibar, wanaikomboa kutoka katika mikono ya nani! Zanzibar hivi sasa inatawaliwa na wazanzibari wenyewe, wanyonge, wavuja jasho, wakwezi na wakulima. Je sasa anayetaka kuondoshwa madarakani ni nani? Na nani awekwe badala yake?

Nadharia hiyo ya kudai ukombozi ndani ya Taifa huru iliibuka katika kipindi kirefu tangu ndani ya mfumo wa chama kimoja cha siasa. ASP na baadae mwaka 1977 CCM. Mjaribio kadhaa yasiofaulu ya kutaka kuipindua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaligundulika moja kati yaayilo ni lile lililopelekea kuuwawa kwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume, Aprili 7, 1972. Mjumuiko wa matukio hayo, ni ishara iliyowazi kwamba athari za siasa za vyama vilivyokuwepo kabla ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 zinaendelea kubaki licha ya vyama hivyo vilivyokuwa vikipigania uhuru kuvunjwa baada ya Mapinduzi hayo. Hivyo wafuasi pamoja na baadhi ya vizazi vyao walikuwa wakiendesha sera za vyama hivyo za kugombania ukombozi.

Kikwazo kikubwa kilichositisha kutimizwa kwa azma hiyo ya wafuasi wa vyama vya kale ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambao kwa muundo wake siojambo linalowezekana kuipindua Serikali ya Zanzibar pekeyeke bila ya kuihusisha Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo jmabo linalohitajika kufikisha lengo hilo ni kuparaganya muungano huo ambapo hila na mbinu mbali mbali za kuuvunja zilipangwa na kutekelezwa, lakini hazikufanikiwa.

Kuja kwa mfumo a vyama vingi nchini 1992 na kuanzishwa kwa chama cha upinzani Zanzibar hasa Chama Cha (CUF), kuliipa nguvu mpya mikakati hiyo kwani mbinu zilizotumika katika kukisimamisha chama hicho, zilikuwa hazina tofauti na zile zizotumiwa kuvisimamisha vyama vya zamani ZNP na ZPPP na hasa Pemba. Wananchi walishurutishwa kujiunga na chama hicho, na walionekanwa kutounga mkono CUF, walitengwa, walisusiwa kununuliwa bidhaa zao, waligomewa kuuziwa bidhaa kwenye maduka na masoko, walitengwa kwenye shughuli za kijamii kama vile misikitini, mazikoni maharusini makazini nk. Walinyimwa hata maji ya kunywa visimani na majumbani. Pamoja na shindikizo zote hizo wapo waliokataa kata kata kuiunga mkono CUF. Watu hao walifanyiwa vitendo vya kinyama kabisa, waling’olewa mazao yao katika mashamba, walihamishwa kwa nguvu katika mitaa, wanaume waliachishwa wake zao na kwa wanawake waliachwa na waume zao, na wengine kufika hata kuwekewa kinyesi cha binaadamu kwenye milango na madirisha ya nyumba zao.

Harakati hizo zilianzishwa na kundi maalum ambalo hapana shaka lina malengo waliyo yakusudia. Mipango hiyo inaweza kuhusishwa naile iliyokuwepo wakati wa kugombania uhuru. Lakini katika kufahamu kwa uwazi chimbuko la yote hayo, ipo haja ya kufahamu mwenendo na muelekeo wa kiongozi mkuu wa kundi hilo kuanzia enzi za kudai uhuru, wakati wa mfumo wa chama kimoja na kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Kiongozi huyo ni Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff ambaye anatarajia tena kuwa mgombea wa Kiti cha Urais wa Zanzibar kwa mara ya nne katika Uchaguzi Mkuu ujao 2010.

KUJULIKANA KWA MAALIM SEIF
Katibu Mkuu wa Chama Cha CUF ambaye anategemewa sana na wafuasi wake, kuna haja kumtiza ma kama kweli ana sifa za mwanasiasa na mwanademokrasia wa kweli. Sief Sharif Hamad alianza kujulikana Zanzibar baada ya Mzee Aboud Jumbe Mwinyi kumteuwa kuwa Waziri wa Elimu mwaka 1977 na baada ya kuunganishwa vyama vya ASP na TANU na kuzaliwa CCM.

Maalim Seiff alikuwa mwalimu katika skuli ya Sayyid Abdalla ambayo hivi sasa inajulikana kwa jina la Fedel Castro, ambapo alikwenda kufundisha mara baada ya kumaliza masomo yake ya kidatu cha sita katka Skuli ya King Geoge hivi sasa inajulikana kwa jina la Skuli ya Sekondari ya Lumumba. Alizaliwa Mtabwe katika kitongoji kinachoitwa Nyali, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, na kupata elimu yake ya msingi katika Skuli ya Uondwe na hatimaye kumaliza masomo yake ya elimu ya juu katika Skuli ya King Geoge.

Mwishoni mwa miaka 1960 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika juhudi ya kuandaa Wataalamu na viongozi wa baadae, iliwapeleka vijana wake nchi za nje kujifunza taaluma mbali mbali. Seif Shariff, alichaguliwa kuwa miongoni mwa wanafunzi hao waliopelekwa kwa ajili ya kuchukua taaluma katika vyuo vya nchi za nje.
Kwa wakati ule wanafunzi wote waliopelekwa nchi za nje walikuwa wanaandaliwa kuwa viongozi na makada watakaoshika nyadhifa mbali mbali za uongozi katika Serkali. Kwa sababu kipindi hicho hakikuwa kirefu tangu kufanyika Mapinduzi yaliyomuondoa Sultan, waliopatiwa nafasi hizo walilazimika waangaliwe kwa kuchunguzwa hasa misimamo yao ya kisiasa.

Seif katika kuchunguzwa itikadi yake ya kisiasa ikabainika alikuwa alikuwa na msimamo wa ki-Hizbu tangu alipokuwa Beit-el-Ras. Akiwa bado mwanafunzi alianzisha Chama cha wazawa wa Pemba mapema mwaka1961, Chama hicho kilitumika katika mpango wa kukipatia kura za udanganyifu Chama cha ZNP (HIZBU) hasa katika Uchaguzi wa mwisho mwaka 1963.

Hali hiyo iliwezekana kutokana na MaalimSeiff kuwa karibu sana na Zaim Ali Muhsin, Maulid Mshangama na Ibun Saleh. Alishiriki mara nyingi katika mikutano ya siri ya ZNP iliyokuwa ikifanywa na Maulid Mshangama wakati huo alipewa tuzo ya kumuoa mtoto wa kifalme aitwae Amal. Walikuwa kila jioni wakienda Beit-EL-Ras kufanya mazoezi ya kutembea ufukweni, huku kila siku Seiff akiwa ndiye aliyekuwa akiwatembeza.

Akishirikiana na Ali Muhsin, Seiff aliwahi kuandaa Maulidi ya Mrtume Muhammad (SAW) Beit-El-Ras 1963 kwa njama ya kuwakutanisha pamoja Ali Muhsin na Mzee Karume, ambaye walimualika na akahudhuria. Baadaye Seiff alitangaza ASP imeungana na ZNP. Pia chama cha Wazawa wa Pemba kilishiriki kikamilifu katika wizi wa kura wa kiti cha Darajani 1961. Wizi huo wa kura ndio uliokuwa sababu na chimbuko hasa la vita vya Juni.

Mwak 1963 wakati ASP ilipojidhatiti kukichukua kiti cha Darajani kwa kumueka mgombea wake Mzee Thabit Kombo. Juma Ngwali kwa kushirikiana na chama cha Wazawa wa Pemba, chini ya uongozi wa Seif Shariff walikabidhiwa meli ya Jamuhuri wakati huo ikiitwa Sayid Khalifa (jina la mmoja kati ya Wafalme waliotawala Zanzibar) kwenda kuchukuwa watu Pemba kwa ajili ya kupiga kura kwa Mgombea wa ZNP, na kiti hicho kilichukuliwa na ZNP. Seif alisikika akijigamba kuwa juhudi zake zimeleta mafanikio.

Kutokana na ushahidi huo, jina la Seiff liliondolewa katika orodha ya wanafunzi waliokwenda kupata mafunzo ya nje ya nchi licha ya kuwa alikuwa ameshafika Unguja kwa safari.

Ilioekana kuwa sio busara kumrudisha tena Pemba, ndipo ilipoamuliwa apelekwe katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba akafundishe. Maalim Seif Shariff aliendelea na kazi ya kufunidisha mpaka mwaka 1972 baada ya kifo cha Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa Zanzibar ambapo nafasi yake ikashikiliwa na Bwana Aboud Jumbe. Katika kipindi cha utawala wake Jumbe, wakati huo Waziri wake wa Elimu akiwa Bwana Said Iddi Bavuai na Naibu Waziri Bwana Aboud Talib, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mara ya kwanza ilipeleka wanafunzi kumi na moja kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar-es Salaam. Waliteuliwa vijana waliofaulu vizuri masomo yao ya kidatu cha sita na kupelekwa Chuoni huko pamoja na vijana hao aliteuliwa na Seiff Sharif yeye akiwa Mwalimu katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba. Vijana hao ni -:
1. Abdalla Ismail Kanduru
2. Abubakar Khamis Bakari
3. Aziza Ali Saidi
4. Iddi Pandu Hassan
5. Juma Duni Haji
6. Mabrouk Jabu Makame
7. Mbarouk Omar
8. Moh’d Mwinyi Mzale
9. Omar Ramadhan Mapuri
10. Said Gharibu Bilali
11. Seiff Sharifu Hamadi

Kama kawaida katika kufanya hadhari ya kuteua vijana, Wizara ya Elimu ilikuwa na kazi kubwa ya kufanya uchaguzi juu ya misimamo yao kisiasa, jambo ambalo lilipelekea wajumbe wa Kamati ya Wizara kubishana, hatimae Mzee Jumbe akashauri kuwa ni vizuri kusahau tofauti zilizokuwepo za kisiasa na waachiwe vijana wapate elimu ili kuja kulitumikia Taifa.

Wakiwa katika mazingira ya Chuo Kikuu, mawazo ya kutaka kuleta mabadiliko ya maendeleo Zanzibar yaliibuka na kuwatawala vijana hao. Hali ya kutoridhika na baadhi ya mwenendo na maamuzi yaliyokuwa yakichukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaliingia katika vichwa vya baadhi yao. Kutokana na hali hiyo, kulijengwa msimamo na vijana hao kwamba yeyote atakayebahatika kapata nafasi ya juu, ajitahidi kuwavuta wenzake ili wasaidiane katika kuleta maendeleo ya haraka.
Baada ya kumaliza masomoa yao, wakiwa wote wamechukuwa shahada ya kwanza ilioambatana na ualimu, isipokuwa watu watatu, Seif Shariff alichukuwa Shahada ya kwanza katika Social Science, Iddi Pandu na Abubakar Khamis wao walichukuwa Shahada ya Sheria. Baada ya kumaliza masomo yao walirejea Zanzibar. Naibu Waziri wa Elimu Bwana Aboud Talibu aliongozana nao hadi kwa Rais Jumbe kwa nia ya kumfahamisha kuwa vijana hao wamemaliza masomo yao na wako tayari kulitumikia Taifa.

Rais Aboud Jumbe kwa sababu alimkumbuka Seiff Sharifu kwani aliwahi kumfundisha King Geoge kabla hajaacha kazi ya ualimu na kujiunga na siasa, aliagiza wale wahitimu kumi wapangiwe kazi na Seiff Sharifu akampa kazi Ikulu. Waliobaki mbali ya waliosomea sheria walipelekwa Chuo cha Ualimu Nkuruma kwa kazi ya kufundisha.
Maalim Seiff alifanya kazi kwa uhodari mkubwa mpaka akafikia cheo cha Katibu wa Rais, hadi mpaka pale alipoteuliwa na Rais Jumbe kuwa Waziri wa Elimu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kwa maana hiyo aliyemfanya ajulikane Maalim Seiff Zanziba, na hatimae Tanzania nzima, ni Mzee Aboud Jumbe. Na alifanya hivyo kwa lengo la kuimarisha umoja na mshikamano wa Wazanzibari.

AKIWA WAZIRA WA ELIMU
Mtu wa kwanza aliyebahatika kupata wadhifa mkubwa miongoni mwa vijan hao alikuwa ni Maalim Seif alipoteuliwa kuwa Waziri wa Elimu mnamo mwaka wa 1977. Kwa kiasi Fulani alitekeleza ahadi waliopeana na wenzake kwani aliwavuta Mbarouk Omar na Omar Ramadhan Mapuri wakiwa ni watu wa karibu yake sana na kutokana na kufahamu kuwa anafanya kazi na wenzake Maalim Seif alianza kujijengea ngome ya kufanya atakavyo kwa kuamini wasaidizi wake hawawezi kumsaliti kutokana na kuwa yeye ndiye aliyewapendekeza kuteuliwa kushika nafasi hizo.

Akiwa Waziri wa Elimu ndipo alipoanza kutekeleza sera za ubaguzi kuwagawa Wapemba na Waunguja . Kila kitu zikiwemo nafasi nyingi za mzsomo zilielekezwa Pemba na kuwapa zaidi jamaa zake hasa wa Mtambwe. Alifanya hivyo kwa kuelewa kuwa Serikali imeweka utaratibu mzima wa kuangalia mgao wa nafasi za masomo ya juu kwa sehemu ya Unguja iliokuwa na wakaazi wengi, kupatiwa nafasi sita (6) na Pemba nne (4) kwa kila nafasi kumi (10) zilizopatikana.
Akiwa Waziri wa Elimu Zanzibar, Maalim Seiff alibadilisha mfumo huo na kuweka nafasi sita kwa Pemba na nne kwa Unguja, tena katika nafasi hizo nne za Unguja, walitafutwa wale wenye asili ya Pemba ambao wanaishi Unguja na kupatiwa nafasi hizo na kukifanya kisiwa cha Unguja kutopata nafasi hata moja.
Alipobaini mpango wake huo huenda ungegunduliwa, alibuni mbinu nyengine ya kuwapeleka masomoni katika vyuo vya Bara vijana wa Pemba kwa kuwapeleka vyuoni moja kwa moja bila ya kuwapitisha Wizarani. Serikali ya Muungano ilipouliza, Maalim Seif kwa niaba ya Zanzibar alithibitisha kuwa wanafunzi hao waliteuliwa kihalali na SMZ.
Na wengi kati ya wanafunzi waliopelekwa kwa mtindo huo walikuwa hawana sifa za kujiunga na vyuo hivyo. Aidha Maalim Seif alidiriki kuwaondoa wafanyakazi wenye nyadhifa za juu katika Wizara ya Elimu wenye asili ya Unguja na kuwashusha vyeo na kuwapa jamaa zake wa Pemba. Hali ilipozidi kuwa mbaya na kuchukiza zaidi baada ya Maalim Seif kuhusika pia na kashfa ya ubadhirifu wa fedha za mradi wa madawati ya Skuli. Ndipo Rais Aboud Jumbe aliparifiwa vlio vya muda mrefu vya wananchi waliokuwa wamechoshwa na vitendo vya upendeleo vilivyokuwa vikifanywa na Maalim Seif. Rais Jumbe alichukuwa hatua ya kumuondoa katika wadhifa wake huo. Kuanzia siku hiyo Maalim Seiff alianza kujenga chuki dhidi ya Mzee Jumbe, kwa kudai kwamba amemuonea kufuatia kumuondoa katika wadhifa wake waWaziri wa Elimu.

No comments: